Tuesday, September 7, 2010

Likizo

Kila mwaka mwezi wa Ramadhan The Kilimanjaro band wananjenje,huwa wanachukua nafasi hiyo kwenda likizo na kupata muda wa kutafakari walikotoka na wanako kwenda. Moja ambalo liko wazi ni kuwa kipindi kirefu kimepita toka wametoa album yao ya mwisho. Kubwa lililokwamisha ni kuwa kila mara bendi imekuwa ikiongoza njia ya mwelekeo wa mtindo wa mduara, ni muhimu kuja na kitu ambacho kitaendeleza utaratibu huu.. Hivyo kuanza kutafakari njia mpya ya mwelekeo wa mduara ndio imelazimika kuchukua muda mrefu kutafakari hili.
Hata hivyo tayari nyimbo mbili zimekwisha anza kupigwa katika maonyesho yake, Nyoka, Manenoneno ambazo zimepokelewa vizuri na wapenzi wa Njenje.

No comments:

Post a Comment